Friday, June 7, 2013

RAIS KENYATTA, AHUTUBIA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI KWA MARA YA KWANZA


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alifanya kikao chake cha kwanza cha baraza la mawaziri huko Nairobi Alhamisi (tarehe 6 Juni), akiwaagiza mawaziri kutimiza ahadi zilizotolewa na Muungano wa Jubilee wakati wa kampeni za uchaguzi.
Aliongeza kwamba watu wanatarajia mabadiliko katika maeneo kama vile utoaji wa huduma, kupunguza umaskini, usalama wa chakula, usalama wa taifa na kupatikana kwa huduma za afya na elimu. Wakati wa mkutan huo, baraza la mawaziri lilipitisha Mswada na Sera ya Usimamizi wa Hifadhi ya wanyamapori ambayo inatoa adhabu kali kwa wote wanaohusika na ujangili, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.

Chini ya Mswada huo, maafisa wa Huduma za Wanyamapori Kenya watakaokamatwa wakishirikiana na majangili wataondolewa katika nafasi zao. Mswada huo pia utatoa faini za hadi shilingi milioni 1 (dola11,800) kwa majangili watakaokamatwa.

Na  Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sheria mpya ya Wanyamapori ikidhamiria kuzuia tishio linalotishia tembo, simba, nyati, vifaru na chui, Capital FM ya Kenya iliripoti Alhamisi (tarehe 23 Mei).
Ruto alipendekeza pia kuongeza bajeti ya utangazaji ya Bodi ya Utalii Kenya kutoka shilingi milioni 740 (dola milioni 8.78 ) hadi shilingi bilioni 3 (dola milioni 35.6).
Ongezeko la bajeti unadhamiria kuongeza mara mbili idadi ya sasa ya watalii milioni 1.6 hadi milioni 3 kwa mwaka. Takriban ndovu 360 na vifaru 19 waliuawa nchini Kenya mwaka 2012.

No comments: