Pigo tena kwa muziki wa Bongo Fleva baada ya Kuondokewa na SHARO MILLIONAIRE miezi michache iliyopita Tasnia ya muziki wa kizazi kipya imepata pigo jingine kwa kuondokewa na wasanii wake wawili kwa mpigo, taarifa kutoka south afrika zinasema baada ya Mangwear kukutwa amefariki hapo jana na msanii mwenzake aliyekuwa ameambatana naye kwenye show zake nchini humo M To The P naye amefariki dunia jijini Johannesburg.
Taarifa kutoka Johannesburg zinaeleza M To The P amefariki dunia baada ya kulazwa katika hospitali ya St. Helen Joseph ambayo mwili wa Mangwear umehifadhiwa. Mangwear na M To The P walisafiri pamoja hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya shoo na
baadaye waliendelea na maisha yao. Lakini jana wakati wanatarajia kurejea nyumbani,
Mangwear alikutwa amefariki dunia chumbani kwake kwa kile kilichotafsiriwa kuwa alikuwa ametumia dawa nyingi za kulevya(Overdose) na M To The P yeye alikutwa akiwa taabani na akakimbizwa hospitalini. Lakini nayeye baada ya muda mfupi alifariki.
No comments:
Post a Comment