Politics

PRESIDENTIAL PREPARATION   -3


Baada ya kumaliza kikao chake na wajumbe watarajiwa wa kamati kuu ya chama, Robert maarufu kama Robby alirudi ofisini kwakwe, na kumkuta secretary wake Anna akiendelea kuchapa kazi kama kawaida. Anna alimsalimu bosi wakena salaam ile ilitikiwa na Robert huku ikifuatiwa na swali, “there is any problem?”Anna alijibu”hakuna tatizo bosi”okey, hakikisha unampigia simu Mr. Minja na umwambie ninamuhitaji ofisini kwangu. Maagizo yale aliyo yaacha Robert yalikubaliwa na Anna, kwa kusema sawa bosi.Robert aliingia ofisini kwakwe na kuendelea nashughuli zake za kutafuta udhamini kwa watu na makampuni mbalimbali ndani na hata nje ya nchi, kwa ajili ya kupata pesa ya kutosha kuwezesha Mheshimiwa Leonard kuingia madarakani.
Kipindi hicho Anna aliendelea kupiga simu ya Mr. Minja bila kupokelewa.Baada ya kujaribu kupiga simu ya Mr. Minja kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote, Atimaye alimpigia simu bosi wake na kumueleza kwamba simu ya Mr. Minja ilikuwa inaita bila majibu.“okey, nitamtafutabaadaye ” Robert  alimjibu Anna, na kuamua yeye mwenyewe kumpigia simu Mr. Minja, simu ile iliyopigwa na Robert  ilipokelewa moja kwa moja na Minja, nilimwagiza Anna akupigie simu, lakini simu yako iliita tu bila kupokelewa, “nikweli mzee nilikuwa na kikao kidogo na wafanyakazi wangu kwa muda wa kama  saa moja hivi” alisema Minja. Aliendelea Robertkuuliza kama kulikuwepo na tatizo lilopelekea Minja kuitisha kikao na wafanyakazi wake  na Minja alimjibu moja kwa moja kwamba walikuwa wakipeana utaratibu tu wa kufanyakazi,” okey, nakuhitaji ofisini kwangu sasa hivi”alisema Robert.
Robert alibaki anawaza kidogo na kukumbuka juu ya utendaji wa bwana Minja ulivyo mzuri kwa kuibua chokochoko za serikali na chama chetu kwa ujumla na kuifanya jamii ya nchi yetu kuliamini sana gazeti lake kuliko chombo kingine chochote cha habari hapa nchini.  Ghafla Anna aliingia ofisini kwa Robert  na kumfanya Robert  ashituke kidogo, “Bosi kuna hili faili la Mr. Kombani linahitaji lisainiwe, ili baadaye alete cheki” Anna alimwambia bosi wake, nakuulizwa kama Kombani alifika ofisini, “hakuweza kufika ila alipiga simu na kusema atakuja baadaye kuchukua hili faili”. Muda huo huo Minja alifika ofisini kwa bwana Robert, na kusalimiwa na Anna, baadaye na kuondoka na faili lake baada ya Robert kulisaini. Robert  alimkaribisha Minja na kumwambia “bwana nimekuitia jambo moja tu, na tena ni la muhimu sana, kipindi hicho Minja alikuwa akimusikiliza kwa umakini sana alichokuwa akikizungumza Robert, nahitaji umchafue Mheshimiwaaaaaa……mlango ulifunguliwa na Anna aliingia na kumwambia Robert  bosi kuna karatasi moja hujaisaini.
JIONI ya siku hiyo Robert alipita kwa mheshimiwa Leornard, na kuonana naye na kumueleza hali halisi jinsi kikaoKilivyoenda na maazimio ya waheshimiwa wajumbe juu ya kikao kile, na kumuleza kwamba wajumbe wote wa kikao wameazimia juu ya kutafuta ufadhili wa kutosha wa kisi cha zaidi ya bilioni 500 za Kitanzania, ili mambo yote yaweze kwenda vizuri, na kusema kwamba hii nchi ni kubwa sana kwa mfano kama uchaguzi mmoja wa ubunge tu IGUNGA mkoani Tabora chama kilitumia Bilioni 6, je, kwa nchi nzima tutatumia pesa kiasi gani? Kutosha kukata kiu ya watu mbalimbali.Maazimio yale yaliungwa mkono moja kwa moja na mheshimiwa Leornard, na kusema sasa itabidi tugawane majukumu katika zoezi la kukusanya fedha, alisema mheshimiwa Leonard. Baada ya mazungumzo ya muda kati ya mheshimiwa Leornard na Robert.  Robert aliamua kuondoka na kurudi nyumbani kwakwe na kumkuta mke wake na mwanaye mdogo wa miaka 5, wakiwa salama na kuingia bafuni kuoga.


PRESIDENTIAL PREPARATION   - 2
Piiiiiiiiiiiiiiiii,piiiiiiiiiiiiiiiiii,piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, ilikuwa ni honi ya gari inapigwa getini kwa mheshimiwa Leornard, na kumfanya mlinzi aende kuchungulia  nani alikuwa anapiga honi  getini. Lakini wakati baba askofu anafika getini kwa mheshimiwa Leornard tayari Alisha mtaarifu kama kafika, wakati mlinzi anachungulia getini, simu yake  ya kibandani iliita na alipoipokea, aliambiwa na mheshimiwa Leornard amfungulie baba askofu. Mlinzi alirudi getini na kumfungulia Baba Askofu. Baada ya kuingia ndani Baba askofu aliegesha gari yake , sehemu ya maegesho ya magari nyumbani kwa mheshimiwa
Leornard na alipo shuka kutoka kwenye gari alimsalimia askari Yule wa getini. Na baada ya salamu askari Yule alimuongoza Baba Askofu mpaka alipokuwa amekaa mheshimiwa Leornard  na Mzee Anthony.

Mheshimiwa Leornard: Oooooh Baba Askofu karibu sana.

Baba Askofu: Asante sana, tumsifu yesu kristo. Mheshimiwa Leornard kwa pamoja na Mzee Anthony: waliitikia milele amina.

Baada ya kujuliana hali za majumbani mwao wote watatu kwa pamoja, Silyvia mfanyakazi wa nyumbani kwa mheshimiwa Leornard alifika na kumsalimu baba askofu, na kumuuliza kinywaji ambacho angependa kutumia, kipindi hicho mheshimiwa na mzee wa kanisa mzee Anthony walikuwa wakiendelea kunywa juice na baba askofu aliomba aletewe maji ya kunywa ili aweze kupooza koo. Baada ya muda mfupi mama Lawrence, mke wa mheshimiwa Leornard alitoka ndani akiwa na maji na kwenda kumuhudumia baba askofu, na kusalimiana kidogo na mama Lawrence alirudi ndani na kumuacha mheshimiwa Leonard, Baba Askofu pamoja na mzee Anthony wakiendelea na mazungumzo yao.

Mzee Anthony; aaaaah Baba Askofu, baada ya misa ya juzi kuona umezungumzia sana swala la michango na sadaka kwa ujumla kwa wauminii……….Baba Askofu: ndiyo ndiyo

Mzee Anthony: nilifikilia sana na kujiuliza maswali mengi ni kivipi kupitia tu sadaka tungeweza kumalizia ujenzi ambao umebakia, tena ambao ni mkubwa kuliko sehemu tuliyojenga, “ni kweli mzee wa kanisa” yalikuwa ni maneno yake baba askofu. Niliamua kumfuata Mheshimiwa Leornard hapa, nikamuelezea hali halisi juu ya sehemu ya ujenzi wa kanisa letu ulipofikia, na yeye kwa upande wake amehaidi kuchangia milioni 100 pesa za kitanzania. Abarikiwe na Mwenyezi Mungu atamlipa alisema baba askofu. Aliendelea mzee wa kanisa kwa kusema, lakini wakati tukiyazungumza haya, shemeji mama Lawrence naye alikuwepo na akashauri kwamba mheshimiwa Leonard ni mtu wa watu anayependwa sana na watu, kwahiyo ingekuwa vyema ahudhurie ibada na kufanya harambee  kwa waumini ili tukamilishe ujenzi wa nyumba ya ibada, naimani waumini wataweza kumsikiliza kiongozi wao kwasababu wanampenda na wanaweza kumalizia kiasi kilichobaki.

Baba Askofu : Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, wazo zuri sana mzee wa kanisa, naimani haya yote ni mapenzi mema ya mwenyezi Mungu juu ya nyumba yake ya ibada. “nikweli baba askofu ”alisema mheshimiwa Leornard. Karibu sanamheshimiwa Leonard kanisani kwetu kwa ajili ya huduma za kiroho na kuwahamasisha waumini juu ya ujenzi wa nyumba yao ya ibada.



 PRESIDENTIAL PREPARATION   -1
Ndani ya siku chache zijazo chama chetu kitakamilisha chaguzi zake za ndani, zoezi ambalo limechukua takribani mwaka mzima, tangu chaguzi za kwenye mashina zilipoanza. Zoezi hili litakapo kamilika katika mkutano mkuu wa chama chetu, chombo ambacho ni cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, kitakuwa na uongozi mpya katika nafasi zote.
Kutakuwepo na viongozi wapya kabisa, watakuwepo na waliorudi na wapo ambao watakuwa wamebadilishwa nafasi zao. Wapo wale ambao licha ya kujaribu sana watakuwa wametupwa kwenye nafasi za uongozi ndani ya chama hata kama wanazo nafasi zao za kiserikali.
Viongozi hawa wapya watakao chaguliwandio watakao kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama chetu, mkutano mkuu wa chama ndicho chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, upo juu ya vyombo vingine vyote , ikiwemo katiba ya chama chetu, kwani ndicho chombo ambacho kinaweza kubadili katiba ya chama bila kuwa na rufaa dhidi yake. Lakini zaidi ni mkutano mkuu ndio ambao unaweza kutengua uamuzi wowote uliowahi kutolewa kipindi cha nyuma na chombo chochote au na mtu yeyote wa chama chetu. Kimsingi mkutano mkuu unaweza kutengua maamuzi ya sekretarieti ya chama au hata ya mwenyekiti wa chama chetu.
Kwahiyo kuelekea uchaguzi huu mkuu lazima kambi yetu ijipange kuhakikisha sekritarieti yote ya chama inatuunga mkono na theluthi mbili ya wajumbe wote wa mkutano mkuu wanakuwa ni wakambi yetu ndani ya chama.
Kwasababu kuelekea uchaguzi mkuu mara baada ya uchaguzi ndani ya chama  chetu ni lazima tutashuhudia kuibuka angalau kwa kambi mbili zaidi, ukiondoa kambi yetu ya mheshimiwa Leornard. Kambi  hizi mbili za ziadazitasabisha msuguano ndani ya chama chetu, kama tulivyo shuhudia katika uchaguzi mkuu wa nchi uliopita. Japokuwa uwezekano mkubwa wa kambi moja kati ya hizi mbili kujitoa ndani ya chama chetu . Hili litategemea jambo moja kubwa, kupatana kwa mheshimiwa Leonard na kambi ya mheshimiwa Seba, endapo tutashuhudia viongozi wetu hawa wakiamua kupatana na hatimaye kusimama pamoja, basi mgombea wa chama chetu ambaye atakuwa ni mheshimiwa Leonard atashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa nchi ujao.

Lakini ukweli ni  kwamba majeraha ya kashifa ya ufisadi hayawezi kuponyeka kwa kukumbatiana au kwa kupiga picha pamoja, majeraha haya kwa mheshimiwa Leonard yamezama sana kiasi kwamba sioni uwezekano wowote wa kambi za chama chetu kuweza kukaa pamoja, ni lazima mwenye nguvu apishwe na atakapopita wanaobakia ni lazima watoke.

Written by: Lincoln Pascal 2012.
Don't miss every Thursday and Monday.
#################################################################################

No comments: