Saturday, May 25, 2013

WATU 90 MBARONI KWA KUSABABISHA FUJO MTWARA


Polisi mkoani Mtwara mpaka kufikia jana jioni  walikuwa wamekamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuawa mkoani Mtwara dhidi ya mradi wa bomba la gesi kuelekea Dar es Salaam.
    Mtwara-Tanzania
Hapo Jumatano, polisi walitumia gesi za machozi kukabiliana na ghasia baada ya waandamanaji kulivunja Daraja la Mikindani linaloiunganisha Mtwara na mkoa wa Lindi, wakachoma moto kiasi cha nyumba 10, ikiwemo inayomilikiwa na mwandishi wa habari Kassim Mikongolo wa Shirika la Utangazaji la Tanzania na ofisi kadhaa za serikali na chama tawala, alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi.
Wenyeji wengi wa huko wamepinga mpango wa ujenzi huo wa bomba la gesi, wakihofia kwamba hawatafaidika na rasilimali hiyo.
Rais Jakaya Kikwete aliyalaani maandamano hayo. "Maliasili, haijalishi inapatikana kwenye mkoa gani, ni mali ya Watanzania wote," alisema kwenye hotuba kupitia televisheni.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania limepelekwa mkoani Mtwara kudhibiti ghasia hizo. na mpaka kufikia jana angalau hali ilionekana kuwa shwari.

No comments: