Wabunge wa Kenya wamesalimu amri madai yao ya kuongezewa mshahara
waliyokuwa wameshayapigia kura, lakini badala yake wakajiwekea posho
kubwa zikiwemo gari za kifahari na mafao ya kustaafu.
Mwezi uliopita, wabunge wa Kenya walijipigia kura ya kupandisha mishahara yao, na kupindua makato yaliyokuwa yameamriwa na Kamisheni ya taifa ya Mishahara na Ujira (SRC).
Walipiga kura hiyo kupuuza amri za SRC na kukaidi maombi ya Rais Uhuru Kenyatta kwamba wawe na uvumilivu, na kuongeza mshahara wao wa mwezi hadi shilingi 851,000 (dola 9,955).
Wanaharakati wamefanya maandamano ya aina hiyo nje ya jengo la bunge katika wiki za karibuni wakiwataka wabunge hao kukata malipo yao, ikiwemo maandamano moja ambapo waliachia Nguruwe na kumwaga damu ya wanyama, imekuwa kawaida kwa waandamanaji wa kenya kutumia nguruwe katika maandamano yao ikiwa kama ishara ya ulafi kwa wabunge wao kama Nguruwe ajulikanavyo alivyo mlafi.
Siku ya Jumanne, waandamanji walicheza na Nguruwe mkubwa wa makaratasi na kupeperusha noti bandia na mabango yaliyoandikwa "MPigs".
Lakini SRC ilisema baada ya mazungumzo "yenye faida" na wabunge, wamekubali kuheshimu amri ya kukatwa kwa mshahara kwa takribani asiimia 40 hadi kufikia shilingi 532,000 (dola 6,222).
Wabunge walikubaliana na mpango huo baada ya kufikia muafaka juu ya ruzuku ya shilling milion 5 za Kenya sawa na shilling milioni 95 za Tanzania(Dola 58,500) kwa ajili ya magari ya kifahari. Ruzuku hiyo ilionekana kuwa 'jambo linalowezekana kuwa yenye mafanikio zaidi' kuliko kumpa kila mbunge gari na dereva wake kwa wabunge wote 416, ilisema SRC.

No comments:
Post a Comment