Somalia yajiunga na Mkataba wa Cotonou
Mkutano wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya na zaidi ya nchi 70 katika Kundi la Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) uliidhinisha maombi ya Somalia kujiunga na Mkataba wa Cotonou Ijumaa (tarehe 7 Juni)."Somalia itafaidika kiasi kikubwa kutokana na hili," alisema balozi wa Somalia kwa Umoja wa Ulaya Nur Adde. "Baada ya miaka 20, Somalia imerudi katika familia ya EU-ACP kama mwanachama kamili. Kujiunga huku kutafungulia Somalia njia mpya, fursa mpya kwa watu wa Somalia."
RAIS KENYATTA, AHUTUBIA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI KWA MARA YA KWANZA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alifanya kikao chake cha kwanza cha baraza la mawaziri huko Nairobi Alhamisi (tarehe 6 Juni), akiwaagiza mawaziri kutimiza ahadi zilizotolewa na Muungano wa Jubilee wakati wa kampeni za uchaguzi.
Chini ya Mswada huo, maafisa wa Huduma za Wanyamapori Kenya watakaokamatwa wakishirikiana na majangili wataondolewa katika nafasi zao. Mswada huo pia utatoa faini za hadi shilingi milioni 1 (dola11,800) kwa majangili watakaokamatwa.
Na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sheria mpya ya Wanyamapori ikidhamiria kuzuia tishio linalotishia tembo, simba, nyati, vifaru na chui, Capital FM ya Kenya iliripoti Alhamisi (tarehe 23 Mei).
Ruto alipendekeza pia kuongeza bajeti ya utangazaji ya Bodi ya Utalii Kenya kutoka shilingi milioni 740 (dola milioni 8.78 ) hadi shilingi bilioni 3 (dola milioni 35.6).
Ongezeko la bajeti unadhamiria kuongeza mara mbili idadi ya sasa ya watalii milioni 1.6 hadi milioni 3 kwa mwaka. Takriban ndovu 360 na vifaru 19 waliuawa nchini Kenya mwaka 2012.
SERIKALI YAENDELEA KUTESA VYAMA VYA UPINZANI.
Polisi wa Djibouti walivamia nyumba ambako wanachama wa chama cha upinzani cha Union for National Salvation (USN) waliokuwa wanakutana katika kitongoji cha Warabaley huko Balbala siku ya Jumapili (tarehe 2 Juni), na kuwatia mbaroni watu 13 akiwemo Rais wa USN Ahmed Youssouf.
Wanachama wa USN waliokamatwa waliachiliwa siku ya Jumatatu
wakisubiri siku ya kufikishwa mahakamani, ambayo bado haijatangazwa.
Tangu kutangazwa hapo tarehe 23 Februari, upinzani umekuwa ukiwahamasisha wanachama wake kuandamana kila Ijumaa, licha ya kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani imewapiga marufuku kufanya hivyo.
katika kujibu maandamano hayo, na kuwashtaki kwa kuchochea vurugu. USN sasa inadai kuwa kuna wafungwa zaidi ya 600 wa kisiasa nchini Djibouti, ingawaje serikali inasisitiza kuwa hakuna hata mmoja.
USN imeendelea kutoa wito wa kufutwa kwa chama cha Union for a Presidential Majority (UMP) kinachoidhibiti serikali, na kuunda hapo mwezi wa Machi bunge sambamba, Bunge Halali la Taifa (ANL), linaloongozwa na Ismail Guedi Hared, kiongozi wa mgombea wa USN katika orodha ya Jiji la Djibouti wakati wa uchaguzi.
"Hofu imeingia makambini," alisema Katibu Mkuu wa USN Abdourahaman Mohamed Guelleh. "Yote hii ni sehemu ya kampeni ya vitisho ya serikali lakini sisi hatutasalimu amri."
"Leo chama cha ANL, ambacho kimeundwa na USN, mshindi wa uchaguzi wa wa tarehe 22 Februari, kinashauriana na watu wa Djibouti katika ngazi ya taifa, "Serikali inatutaka tusizungumze na watu ambao walituchagua na kutuunga mkono."
Mbunge wa UMP Houssein Ali alisema kuwa USN inahitaji kukubali kushindwa. "Uchaguzi umemalizika na UMP imeshinda uchaguzi -- upinzani haina chochote cha kupendekeza kwa watu wa Djibouti isipokuwa kuandamana mitaani."
"Kila wakati ambapo chama cha kisiasa kinapotaka kuandamana, wanataka waandamane katika Wizara ya Mambo ya Ndani," aliiambia Sabahi. "Na sehemu za kuabudia kwa mfano huu, misikiti kwa hali yoyote haiwezi kuwa jukwaa la shughuli za kisiasa au maandamano bila ya adhabu kali chini ya sheria ya jinai."
Moktar Abdi, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Djibouti, alisema vyama vyote vinahitaji kukaa meza moja ili kuzungumza na kuafikiana kwa faida ya jumla ya taifa.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>Tangu kutangazwa hapo tarehe 23 Februari, upinzani umekuwa ukiwahamasisha wanachama wake kuandamana kila Ijumaa, licha ya kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani imewapiga marufuku kufanya hivyo.
katika kujibu maandamano hayo, na kuwashtaki kwa kuchochea vurugu. USN sasa inadai kuwa kuna wafungwa zaidi ya 600 wa kisiasa nchini Djibouti, ingawaje serikali inasisitiza kuwa hakuna hata mmoja.
USN imeendelea kutoa wito wa kufutwa kwa chama cha Union for a Presidential Majority (UMP) kinachoidhibiti serikali, na kuunda hapo mwezi wa Machi bunge sambamba, Bunge Halali la Taifa (ANL), linaloongozwa na Ismail Guedi Hared, kiongozi wa mgombea wa USN katika orodha ya Jiji la Djibouti wakati wa uchaguzi.
"Hofu imeingia makambini," alisema Katibu Mkuu wa USN Abdourahaman Mohamed Guelleh. "Yote hii ni sehemu ya kampeni ya vitisho ya serikali lakini sisi hatutasalimu amri."
"Leo chama cha ANL, ambacho kimeundwa na USN, mshindi wa uchaguzi wa wa tarehe 22 Februari, kinashauriana na watu wa Djibouti katika ngazi ya taifa, "Serikali inatutaka tusizungumze na watu ambao walituchagua na kutuunga mkono."
Mbunge wa UMP Houssein Ali alisema kuwa USN inahitaji kukubali kushindwa. "Uchaguzi umemalizika na UMP imeshinda uchaguzi -- upinzani haina chochote cha kupendekeza kwa watu wa Djibouti isipokuwa kuandamana mitaani."
"Kila wakati ambapo chama cha kisiasa kinapotaka kuandamana, wanataka waandamane katika Wizara ya Mambo ya Ndani," aliiambia Sabahi. "Na sehemu za kuabudia kwa mfano huu, misikiti kwa hali yoyote haiwezi kuwa jukwaa la shughuli za kisiasa au maandamano bila ya adhabu kali chini ya sheria ya jinai."
Moktar Abdi, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Djibouti, alisema vyama vyote vinahitaji kukaa meza moja ili kuzungumza na kuafikiana kwa faida ya jumla ya taifa.
KENYA KUFUTA KESI YA KENYATTA & RUTO ICC
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya
Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kwa kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu (ICC) dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine kwa madai
ya dhima yao katika ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007 hadi
2008,liliripoti shirika la habari la AFP.
Bw. Ki-moon alitembelea mji mkuu wa Rwanda Kigali siku ya ijumaa, siku moja baada ya kutembelea nchi za maziwa makuu, na kutangaza mpango mpya wa kumaliza mgogoro wa utajiri wa madini unaoendelea kwa muda mrefu sasa huko mashariki mwa DR Congo ambako wanatumia mpaka na Rwanda.
Tarehe 11/2/2013 nchi za Africa zilisaini mkataba wa amani kwa ajili ya kumaliza mgogoro mashariki mwa Congo, ambao ulilenga kuanzisha jeshi maalum la umoja wa mataifa kwa ajili ya kupambana na makundi ya kiharamia.
Mpango huo unanafasi kubwa kwa kuleta amani kwa miaka mingi, Ban Ki-moon aliwambia waandishi wa habari mjini Kigali. Ninawasihi viongozi wote kila mmoja kufanya kazi yake, Rwanda imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kukomesha vitendo kama vinavyoendelea Congo.
Kutoka Kigali, Ban alisafiri mpaka Entebe Uganda alipo kutana na Rais wa Uganda Yoweri Mseven.Katibu mkuu huyo wa umoja wa mataifa alisema, Rais wa Uganda alimwakikishia kwamba mazungumzo ya amani kati ya M23 na serikali yataendelea Jijini Kampala.
“Watu wa DR Congo wamehangaika kwa muda mrefu sasa, wamechoka na vita, wamechoka na umasikini, wamechoka na kuhamahama,” Ban Ki-moon aliwaambia waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano mjini Entebbe.Jeshi la Umoja wa mataifa, ambalo lilithibitishwa na baraza la usalama mwezi march, lina wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi na Afrika kusini.
Makundi ya Majeshi mbalimbali likiwemo jeshi la M23 yapo mashariki mwa Congo yakipambana kuzuia matumizi ya rasilimali ya madini kama vile Dhahabu ambayo inatumika kutengenezea vifaa mbalimbali mbali vya kielectronic zikiwemo simu, n.k.
Tangu mwanzoni mwa mwaka jana May 2012, watu karibu milioni 3 wamepoteza makazi yao mashariki mwa DR Congo, lakini watu milioni 2.5 wameendelea kubakia hapohapo DR Congo wakati watu 460,000 wameyakimbia makazi yao na kwenda kupata hifadhi nchi jirani za Rwanda na Uganda. Congo DR, Imekubwa na matatizo mfululizo kwa zaidi ya miongo kadhaa sasa, na kusababisha kukuwa kwa umasikini, uharibifu wa miundo mbinu na vita kuendelea kushamili mashariki mwa nchi tangu mwaka 1998 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 5.5.
No comments:
Post a Comment