Langa pumzika kwa amani, Langa kileo ni mwanaharakati wa siku nyingi katika muziki wa hip hop hapa nchini, akiwa ameibuliwa na Coca cola, akiwa ni miongoni mwa wasanii watatu watanzania waliokuwa wakiwakilisha kundi la wakilisha. Umauti umemkumba leo akiwa hospital ya Taifa muhimbili kwa kile kilichosemekana, Langa alikimbizwa hospitalini hapo akiwa na malaria kali iliyopelekea umauti wake.
Serikali yetu inalaumiwa kwa hili kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti ugonjwa huu wa malaria ambao unaendeleza kuteketeza watanzania wengi, kukiwepo ripoti mbalimbali zinazoelezea kuripotiwa kwa vifo vya watanzania wengine zaidi ya ishirini huko Kagera mwezi mei.
No comments:
Post a Comment