Kwa kuanza na tunatoa pole kwa watanzania kwa msiba waliopata leo wa Kijana wao Langa Kileo, alimaarufu kama Langa aliyefariki Jioni ya saa 11, leo tarehe 13/06 /2013 katika hospitali ya Taifa muhimbili alikopelekwa tangu juzi wakati akiwa anaumwa, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amen,
Kabla ya mshituko uliowapata Watanzania kwa Msiba wa Langa Watanzania wengi walikuwa wakifuatilia kwa karibu badget ya nchi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 iliyokuwa ikiwasilishwa na mh. waziri wa fedha Dr. William Augostao Mgimwa, Leo Bungeni mjini Dodoma. Tofauti na matarajio ya walio wengi Bajeti hiyo iliyosomwa na Dr. Mgimwa kwa zaidi ya masaa 2, imeonekana kutokuwa na jipya lolote pamoja na kupigiwa makofi na waheshimiwa wabunge, jumla ya fungu la bajeti ni zaidi ya Trioni 18, shilingi za kitanzania, Fedha kwa ajili ya maendeleo zikiwa ni Trioni 5, na Trioni 4 ikiwa ni Mishahara ya wafanyakazi na Trion 9 kwa ajili ya matumizi mengine,
Bajeti hiyo imeonekana kuzidi kumkandamiza mnyonge kwa kumwachia bei ile ile ya mafuta ya Taa huku Petroli na Diesel zikizidi kupanda, Bajeti hiyo imeshindwa kuwa na ufumbuzi mpya wa vyanzo vya mapato kwa kuendelea kupandisha kodi kwenye Pombe, Sigara, na Vinywaji baridi, huku maji ya viwandani kodi ikibaki pale pale. Bajeti hiyo imezidi kupandisha kodi za leseni za magari kwa mwaka, na kusikiliza kilio cha mbunge wa Tanga mjini mh. Nundu kutowawekea kodi bodaboda na bajaj. Kwa mitizamo ya wengi wizara hii ya fedha na serikali kwa ujumla wameshindwa kutumia vizuri madini, utalii, mawasiliano na rasilimali nyingine kama vyanzo vikuu vya mapato na kusababisha kuendelea kuwepo mwanya mkubwa kati ya walionacho nawasionacho.
written by: Lincoln Pascal
No comments:
Post a Comment