Friday, June 14, 2013

KENYA KAMA TANZANIA, ARV'S, PARACETAMO NA DAWA ZA TB ZOTE FEKI


Wafanyakazi wa vituo vya afya vya Kenya walalamikia ongezeko la matumizi ya dawa bandia zinazouzwa nchini kote, wakitoa wito kwa serikali kuchukuliwa hatua haraka kusimamisha mzunguko wake.
  • Mfanyakazi wa tiba wa serikali akikagua zana za kupima VVU. Mwaka 2012, serikali ya Kenya ilitangua aina hizi za zana kutoka kwenye kliniki zinazoendeshewa na serikali. [Tony Karumba/AFP] Mfanyakazi wa tiba wa serikali akikagua zana za kupima VVU. Mwaka 2012, serikali ya Kenya ilitangua aina hizi za zana kutoka kwenye kliniki zinazoendeshewa na serikali. [Tony Karumba]
"Tunatumia mamilioni katika kurekebisha usugu wa magonjwa kama vile malaria, kifua kikuu kwa sababu wagonjwa bila kujua wanachukua dawa hizi za [bandia], ambazo zina kiwango kidogo au hazina kabisa thamani ya kitiba kwa ajili ya kuwatibu," Nyaim aliiambia Bongo Politics. "Hili linasababisha usugu wa ugonjwa, ikiwalazimisha kulipa fedha zaidi kwa ajili ya kupata dozi yenye nguvu kuhimili magonjwa hayo."
Kwa mujibu wa Bodi ya Utengenezaji na Utoaji Dawa na Sumu (PPBK), dawa bandia ni dawa zisizo na kiwango ambazo zimewekwa nembo za udanganyifu au zinakuwa na viambato vya uongo, ambapo dawa bandia hazina viambato vyenye nguvu.
PPBK imepewa mamlaka ya kuhakikisha kwamba bidhaa zote za dawa zinazotengenezwa ndani ya nchi, kuingizwa kutoka nje ya nchi au kusafirishwa nje ya Kenya zinakidhi viwango vya usalama. Bodi pia inatoa leseni kwa dawa na kusajili wafamasia.
Inakadiriwa kwamba asilimia 30 ya dawa zilizouzwa nchini Kenya mwaka uliopita zilikuwa bandia, zinazosababisha hasara kila mwaka ya zaidi ya shilingi bilioni 10 (dola milioni 117), takwimu za PPBK zilionyesha.
"Tunalielewa tatizo, hata hivyo hili halimaanishi kwamba hatufanyi kazi na kwamba tumeshindwa kuifanya nchi iondokane na bidhaa za dawa bandia za matibabu," mwenyekiti wa PPBK Kipkerich Kosgey aliiambia Bongo Politics.
"Kuanzia Januari, tutawaongezea nguvu wafanyakazi kuimarisha ofisi zetu za vituo vya mpakani ambazo zinatumiwa kama eneo la kuingizia kwa wasambazaji wa dawa," alisema. "Pia tunaongeza uchukuaji wa hatua kali za kinidhamu kuhusiana na maduka ya dawa yasiyosajiliwa katika nchi kwa sababu tunashuku vituo hivi vinawajibika kwa kuuza dawa bandia."

Adhabu kali, utambuzi mkubwa vinahitajika

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Waganga wa Meno cha Kenya Victor Ng'ani alisema dawa bandia zilikuwa zinaathiri uwezo wa wanachama kufanya kazi zao.
"Madaktari wanatoa utambuzi sahihi wa ugonjwa na kuagiza dawa maalumu kutibu ugonjwa fulani, lakini mgonjwa anapokwenda kwenye duka la dawa na anapewa dawa isiyo ambayo inasababisha hatari kwa afya yake, [madaktari] wanalaumiwa na wakati mwingine kuonekana kutomudu kazi yao," Ng'ani alisema.
Kama hali hii itaendelea, alisema, inaweza kusababisha kukosekana kwa ujasiri kwa madaktari na katika mfumo wao wa uangalizi wa afya kwa ujumla na kuwahamasisha watu kutegemea zaidi katika dawa ambazo hazijabadilishwa na huduma za nyumbani.
"Kama chama, tunaona kwamba wote wenye mamlaka ya kukagua ubora wa dawa na kudhibiti uingiaji wa dawa hizi nchini Kenya wamelala kazini, wakiacha maisha ya Wakenya katika huruma ya wanaouza ambao wanavuna mabilioni kutokana na biashara hii haramu," alisema.
Sheria dhaifu za kuzuia ughushi, gharama kubwa za dawa halisi na kukosekana kwa uelewa miongoni mwa jamii kuhusu jinsi ya kutambua dawa bandia kunaendeleza biashara hii haramu, alisema Ng'ani.
Kama suluhisho, alisema, serikali inapaswa kuweka adhabu kwa wale watakaokutwa wakitoa dawa bandia, pamoja na kuanzisha kanuni nzuri zaidi kwa maduka ya dawa na wadau wengine.
"Watu wanaouza dawa hizi wanahatarisha maisha ya watu na hata kusababisha kifo. Kila wanapokamatwa, [wakijaribu] kushitakiwa kwa mauaji wanapaswa kutozwa dhidi yao na sio tozo za ughushi tu, ambao [unawaruhusu] kuendelea kufanya kazi baada ya kulipa faini ya chini ya shilingi 200,000 (Dola 2,340)," alisema.
Adhabu hizo za uzembe zinawahamasisha washitakiwa kuendelea na shughuli zao baada ya kushitakiwa, alisema, akiongeza kwamba mamlaka zinapaswa kuongeza uchunguzi wa biashara zinazouza dawa na vifaa vya tiba na kukagua usambazaji wake na rekodi za mauzo.
Dawa zenye thamani kubwa kama vile viuavijasumu na dawa za kutibu malaria, shinikizo la damu, VVU/UKIMWI, kansa na kisukari ni dawa ambazo zinaghushiwa zaidi, alisema Ng'ani, pamoja na baadhi ya dawa za kawaida kama vile dawa za kutuliza maumivu.

Kuzuia aina za dawa na kuziba mianya

Dawa nyingi za bandia, ambazo wafamasia wasio na leseni wanauza, kimsingi wanajinufaisha kwa kusambaza katika vituo vya afya vya serikali kwa kuwatumia wafanyakazi wasiokuwa waaminifu, alisema Nyaim, mwenyekiti wa KMA.
Alitoa wito kwa PPBK kupunguza idadi ya aina za dawa kwa kuziba mianya inayoruhusu wanaoghushi kupenyeza bidhaa zao nchini.
"Kuwa na aina mbili au tatu za parasetamo kutasaidia kurahisisha ufuatiliaji, kutambua na kuzigundua ambazo hazijaidhinishwa, lakini kama ilivyo sasa ambako kila aina inaweza kuingia sokoni, ni vigumu," alisema Nyaim.
Mwezi Aprili, PPBK ilizindua mfumo wa mtandaoni unaoruhusu wagonjwa na wafanyakazi wa sekta ya afya kutoa taarifa kuhusu dawa za kiwango cha chini au ambazo zinaweza kusababisha madhara baada ya kuzitumia. Vituo vyote vya afya vya serikali nchini vinashirikiana taarifa hizi, kusababisha uraisi wa kufuatilia na kutenga dawa zisizofaa, alisema mwenyekiti wa bodi Kosgey.
Bodi inapanga kuzungumza na Tume ya Utekelezaji wa Katiba ili kutafuta njia za kubadilisha sheria zinazoshughulikia dawa bandia na kuweka adhabu kali dhidi ya wavunjaji, alisema.
Alisema shirika lake pia lilifikishwa mbele ya polisi na majaji kuwapa taarifa kuhusiana na aina mbalimbali za biashara. "Mfumo uliopo wa haki za uhalifu unahitaji kuwa makini na nini maana ya ughushi wa biashara kwa nchi na kwa nini wanahitaji kushughulikia kukomesha biashara hii," alisema Kosgey.

No comments: