Friday, June 14, 2013

MUIGIZAJI MASELE CHA POMBE ANUSURIKA KIFO NA KUSABABISHA KIFO.

Masele msanii maarufu wa kundi la vituko show lenye maskani yake hapa mjini Tanga, jana majira ya saa 6 mchana alinusurika kifo baada ya kusababisha ajali inayosemekana kupelekea kifo cha mtu mmoja, katika junction ya makorora hapa jijini Tanga.
 
Masele alikuwa akiendesha gari aina ya pajero mini na baada ya kufika katika junction hiyo ya makorora aliingia mmoja kwa moja bila kusubilia magari na pikipiki zilizokuwa zikitokea highway na kupelekea kusababisha ajalia ambapo mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda akitokea madina aliyeonekana akitembelea speed 100 kilisema chanzo chetu, aligonga gari ya Masele aliyekuwa ameingia vibaya na bodaboda huyo kupoteza maisha hapo hapo, na Masele baada ya kuona ajali imetokea aliamua kung'ang'ania ndani ya gari huku akionekana kuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa naye kwenye gari na kupelekea wananchi kuvunja kioo cha gari lake na Masele kutoka na kukimbilia Nyumba ya jirani, na baada ya muda mfupi polisi walifika na kumnusuru Masele na kuondoka nayekuelekea kituo kidogo cha polisi mabawa.

No comments: