Piiiiiiiiiiiiiiiii,piiiiiiiiiiiiiiiiii,piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,
ilikuwa ni honi ya gari inapigwa getini kwa mheshimiwa Leornard, na
kumfanya
mlinzi aende kuchungulia nani alikuwa
anapiga honi getini. Lakini wakati baba
askofu anafika getini kwa mheshimiwa Leornard tayari Alisha mtaarifu kama
kafika, wakati mlinzi anachungulia getini, simu yake ya kibandani iliita na alipoipokea, aliambiwa
na mheshimiwa Leornard amfungulie baba askofu. Mlinzi alirudi getini na
kumfungulia Baba Askofu. Baada ya kuingia ndani Baba askofu aliegesha gari yake
, sehemu ya maegesho ya magari nyumbani kwa mheshimiwa
Leornard na alipo shuka
kutoka kwenye gari alimsalimia askari Yule wa getini. Na baada ya salamu askari
Yule alimuongoza Baba Askofu mpaka alipokuwa amekaa mheshimiwa Leornard na Mzee Anthony.
kumfanya
mlinzi aende kuchungulia nani alikuwa
anapiga honi getini. Lakini wakati baba
askofu anafika getini kwa mheshimiwa Leornard tayari Alisha mtaarifu kama
kafika, wakati mlinzi anachungulia getini, simu yake ya kibandani iliita na alipoipokea, aliambiwa
na mheshimiwa Leornard amfungulie baba askofu. Mlinzi alirudi getini na
kumfungulia Baba Askofu. Baada ya kuingia ndani Baba askofu aliegesha gari yake
, sehemu ya maegesho ya magari nyumbani kwa mheshimiwa
Mheshimiwa Leornard: Oooooh Baba Askofu karibu sana.
Baba Askofu: Asante sana, tumsifu yesu kristo. Mheshimiwa
Leornard kwa pamoja na Mzee Anthony: waliitikia milele amina.
Baada ya kujuliana hali za majumbani mwao wote watatu kwa
pamoja, Silyvia mfanyakazi wa nyumbani kwa mheshimiwa Leornard alifika na
kumsalimu baba askofu, na kumuuliza kinywaji ambacho angependa kutumia, kipindi
hicho mheshimiwa na mzee wa kanisa mzee Anthony walikuwa wakiendelea kunywa
juice na baba askofu aliomba aletewe maji ya kunywa ili aweze kupooza koo.
Baada ya muda mfupi mama Lawrence, mke wa mheshimiwa Leornard alitoka ndani
akiwa na maji na kwenda kumuhudumia baba askofu, na kusalimiana kidogo na mama
Lawrence alirudi ndani na kumuacha mheshimiwa Leonard, Baba Askofu pamoja na
mzee Anthony wakiendelea na mazungumzo yao.
Mzee Anthony; aaaaah Baba Askofu, baada ya misa ya juzi
kuona umezungumzia sana swala la michango na sadaka kwa ujumla kwa wauminii……….Baba
Askofu: ndiyo ndiyo

Mzee Anthony: nilifikilia sana na kujiuliza maswali mengi ni
kivipi kupitia tu sadaka tungeweza kumalizia ujenzi ambao umebakia, tena ambao
ni mkubwa kuliko sehemu tuliyojenga, “ni kweli mzee wa kanisa” yalikuwa ni
maneno yake baba askofu. Niliamua kumfuata Mheshimiwa Leornard hapa,
nikamuelezea hali halisi juu ya sehemu ya ujenzi wa kanisa letu ulipofikia, na
yeye kwa upande wake amehaidi kuchangia milioni 100 pesa za kitanzania.
Abarikiwe na Mwenyezi Mungu atamlipa alisema baba askofu. Aliendelea mzee wa
kanisa kwa kusema, lakini wakati tukiyazungumza haya, shemeji mama Lawrence
naye alikuwepo na akashauri kwamba mheshimiwa Leonard ni mtu wa watu
anayependwa sana na watu, kwahiyo ingekuwa vyema ahudhurie ibada na kufanya
harambee kwa waumini ili tukamilishe
ujenzi wa nyumba ya ibada, naimani waumini wataweza kumsikiliza kiongozi wao
kwasababu wanampenda na wanaweza kumalizia kiasi kilichobaki.
Baba Askofu : Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, wazo
zuri sana mzee wa kanisa, naimani haya yote ni mapenzi mema ya mwenyezi Mungu
juu ya nyumba yake ya ibada. “nikweli baba askofu ”alisema mheshimiwa Leornard.
Karibu sanamheshimiwa Leonard kanisani kwetu kwa ajili ya huduma za kiroho na
kuwahamasisha waumini juu ya ujenzi wa nyumba yao ya ibada.
No comments:
Post a Comment