Thursday, May 30, 2013

KIKAO CHA BUNGE CHA HAIRISHWA KWA MARA YA PILI HUKO MAKAO MAKUU YA TANZANIA BUNGENI DODOMA.

Naibu speaker wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Job Ndugai amerihairisha bunge kwa mara ya pili leo hii majira ya saa 11:30 jioni huko mkoani dodoma, baada ya Mheshimiwa Ezekia Wenje mbunge wa Chandema na msemaji rasmi wa kambi ya upinzani katika wizara ya mambo ya nje. kwa kile kilichotafsiriwa kwamba kakidharilisha chama cha wananchi CUF wakati akiwasilisha makadrio ya bajeti ya wizara ya mambo ya nje kwa kambi ya upinzani mapema leo asubuhi mjini dodoma.
malalamiko hayo yalitolewa leo asubuhi na wabunge mbalimbali wa CUF na kupelekea naibu speaker kuharisha kikao kwa mara ya kwanza leo asubuhi kwa ajili ya hoja hizo zilizo lalamikiwa na wabunge kwenda kujadiliwa kwenye kamati ya maadili na kumwamuru mheshimiwa Wenje aombe msamaha chama cha wananchi CUF na kuondoa maneno yaliyotumiaka yaliyotafsiliwa kwa kusema kwamba chama hicho cha CUF kinaunga itikadi za ushoga na usagaji, maneno hayo yaliyo someka katika fungu la 3 la hoja hiyo ya kambi ya upinzani yaliamruliwa na kamati ya maadili yaondolewe na Wenje achukuliwe hatua za kindhamu lakini kiti cha naibu spika kilimtaka Wenje aombe radhi chama cha CUF na kutosoma fungu la 3, kitu ambacho kilipelekea Wenje atoe uthibitisho kwa kile anacho kisema na kuendelea kusisitiza kwamba kwa kuwa alikuwa akizungumza ukweli mtupu hana sababu ya kuomba msamaha wala kuondoa maneno hayo. Baada ya mvutano wa muda mrefu mchana huu wa leo Wenje alikubali kuondoa fungu la 3 bila kuomba msamaha na kumfanya naibu spika Job Ndugai kuhairisha bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi ambapo itasomwa bajeti ya wizara ya mifugo.

No comments: