Monday, May 6, 2013

JESHI LA POLISI JIJINI ARUSHA LIMETHIBITISHA KUTOKEA KWA VIFO VYA WATU WATATU NA WENGINE 61 KUJERUHIWA KUFUATIA MLIPUKO

Jeshi la Polisi jijini Arusha limethibitisha kutokea kwa vifo vya watu watatu na wengine 61 kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu katika Kanisa la Mtakatifu Yoseph Mfanyakazi Olasiti lililokuwa lizunduliwe na Balozi wa Vatican nchini Tanzania Francis Kadida. 
Mlipuko huo umetokea jana Majira ya saa tano asubuhi ambapo mashuhuda wa tukio hilo akiwemo RICHARD KOPLO na HILDA MASUWE wamedai kumuona mtu mmoja akitupa kitu kanisani hapo na kukimbia huku akipiga kelele za mwizi. Kwa upande wake Kamanda wa Ploisi wa Mkoa wa Arusha LIBERATUS SABAS amesema, kufuatia tukio hilo wameanza uchunguzi kuwabaini waliohusika ili wachukuliwe hatua kali za kisheria. Kwa ujumla tukio hilo la kushtukiza limegusa hisia za watu wengi, kwa kuliona hilo Mkuu wa Arusha Magesa Mulongo anatoa wito kwa jamii kuwa na subira na subira wakati Jeshi la Polisi likifanya uchunguzi kuwabaini wanaohusika. Kufuatia hali hiyo Msaidizi wa Askofu Jimbo la Kaskazini Padre TENGE amelazimika kuharisha uzinduzi wa Kanisa hilo Jipya lililo chini ya Parokia ya Burka ili kuhakikisha usalama wa waumini na majeruhi.

No comments: