Tuesday, June 11, 2013

OLIVER, MLIPUKO WA MALARIA TANZANIA UKO KWENYE MAENEO AMBAYO HAYAJAPULIZWA DAWA.

Mlipuko wa hivi karibuni wa malaria mkoani Kagera, Tanzania, ulikuwa tu kwenye vijiji ambavyo havikujumuishwa kwenye Programu ya Kupuliza Dawa Majumbani.

Serikali ya Tanzania imetuma timu ya wataalamu kuchunguza mlipuko wa malaria katika mkoa wa Kagera,
Zaidi ya watu 20, hasa watoto, walifariki kwa sababu ya malaria mkoani Kagera kutoka mwishoni mwa Mei.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Seif Rashid alisema serikali imeagiza tiba zadi kutumwa katika hospitali ya Rubya katika wilaya ya Muleba, ambapo wagonjwa wapya wa malaria 30 hadi 40 huripotiwa kila siku.
"Tuna dawa za Alu za kutosha kudumu kwa siku 280 na quinine kwa siku 30 kwenye hospitali ya Rubya ambako mlipuko wa malaria umeripotiwa kutoka tarehe 25 Mei, mwaka huu," Rashid alisema, akipinga fununu za uhaba. "Tunafanya kila kitu kuokoa wananchi na hali iko chini ya udhibiti."
Irenei Kiria, Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya uhamasishaji wa afya ya Sikika, alisema kulikuwa na uhaba wa dawa za malaria kulikosababishwa na uzembe wa wizara katika kununua dawa za kutosha kutoka nje.
"Hili ni suala linalohitaji umakini na tunatoa wito kwa wizara kulishughulikia haraka kwa sababu hakuna sababu za watu kufa kutokana na malaria au kwa ukosefu wa dawa," alisema.
 ambao umeshaua kiasi cha watu 20, wengi wao watoto wadogo, tangu mwishoni mwa mwezi Mei. Vile vile, Wizara ya Afya, imeagiza dawa zaidi kutumwa kwenye hospitali ya karibu ya Rubya, ikikanusha taarifa kwamba mlipuko huo ulisababishwa na upungufu wa vidonge vya kupambana na malaria.
Kila siku kiasi cha watu 30 hadi 40 hufika Hospitali ya Rubya wakiwa na malaria. Wastani wa mtoto mmoja hadi wawili hufa kila siku, alisema Afisa wa Matibabu Hospitali ya Rubya, Diocles Ngaiza. "Katika siku ya kwanza ya mlipuko, vilirikodiwa vifo 16, vingi vikiwa vimesababishwa na watoto hao kufikishwa hospitalini ikiwa wameshachelewa sana,".

No comments: