Wednesday, June 12, 2013

HAYA NDIYO MADUDU YALIYOMO KWENYE RASMU YA KATIBA YA JAJI WARIOBA.

Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar

Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata miundo ifuatayo:
  • Nchi inatawaliwa na serikali ya muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.
  • Tanganyika au Tanzania bara haina serikali wala bunge la pekee.
  • Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake vinavyoratibu mambo yasiyo ya muungano.
Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa shughuli za muungano:

  • Mambo ya nje
  • Jeshi
  • Polisi
  • Mamlaka ya dharura
  • Uraia
  • Uhamiaji
  • Biashara ya nje
  • Utumishi wa umma
  • Kodi ya mapato, forodha
  • Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu






    RASIMU YA KATIBA NA MADUDU YAKE.
  • Muundo wa serikali Tatu, Serikali ya shirikisho,serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar, hii ni kuibebesha mzigo serikali ya Tanganyika kuhudumia serikali mbili zenye ukubwa sawa. Yaani serikali ya Tanganyika yenyewe na serikali ya Muungano. Maamuzi sahihi ilikuwa ni kuvunja muungano au iwepo serikali moja tu na wala si vinginevyo, hili dudu halipiti.

  • Umri wa kugombea Urais bado ni changamoto kwa vijana tena ambao ndio wengi katika Taifa ili, inatakiwa uwe miaka 30 na si 40 kama tume yako ilivyo pendekeza, kijana wa miaka 30 anauwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo kuliko mtu mwenye umri zaidi ya miaka 50, wanasayansi wanaeleza, jambo hili usitegemee kupita kwa vijana ambao ni 70% ya Watanzania wote.
  • Madaraka ya Rais bado ni makubwa sana, kumteua jaji mkuu, naibu jaji mkuu, mwanasheria mkuu, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma hiyo ni kweli tena bila kipingamizi, kitendo cha kuwepo kamati maalum yakupendekeza majina ya watu hawa tena yapelekwe kwa rais ateue hii si sawa hata kidogo katika ufanisi na kutekeleza matakwa ya uongozi bora, viongozi hawa wote wa juu kabisa katika mihimili yetu haitakawi Rais aweke mkono wake hata kidogo zaidi ya kuwaapisha tu, wateuliwe na vyombo maalum na tena waende kuapa kwa rais. Na rais asiwe na mamlaka ya kuwafukuza kazi. kioja cha jaji mkuu kuthibitishwa na bunge, hivi kweli Warioba ulisitahiri kuwa jaji mkuu kweli? kama hujui kwamba mahakama ni muhimili sasa ulikuwa jaji mkuu wa kitu gani? yaani mhimili mmoja uidhinishe mhimili mwingine? kweli? ama kweli ukistaajabu ya Kikwete utayaona ya Warioba,
  • Ubunge wa kurithi, kwamba mbunge mmoja akifariki aliyekuwa akishindana naye kwenye chama achuke nafasi, ilikuokoa gharama za uchaguzi....Tume ya katiba kwa hili akili zenu zilienda likizo, mnataka tuanze kushuhudia vifo vya wabunge kila siku? huu ni upumbavu hakuna uongozi wa hivyo, na raia watakuwa na haki ya kumwita kiongozi wao huyo aliyerithi mikoba? wewe Warioba ni mganga nini?
  • Stay tune, tutaendelea kuwaletea uchambuzi wa madudu yaliyomo kwenye rasmu ya katiba ya Warioba.

No comments: