Kwa uchache raia watatu waliuawa katika mitaa nje ya majengo hayo
wakati majeshi ya Somalia na Umoja wa Afrika yalipojaribu kuingia ndani
katika majengo hayo ili kumaliza kuzingirwa kwa saa moja na nusu, AFP
iliripoti na kuongezea kwamba wakandarasi watatu wa kigeni na kiasi cha
walinzi wa usalama wawili wa Somalia waliuawa wakati wa shambulio hilo.
Shambulio hilo lilianza mnamo saa 10:30 asubuhi saa za eneo hilo wakati gari la al-Shabaab lililokuwa limejaa milipuko lilipolipuliwa nje ya milango ya eneo la UN katka wilaya ya Hodan ya Mogadishu, kwa mujibu wa wafanyakazi wenyeji wa UN waliozungumza na Eroman Informations.
Wapiganaji sita wa al-Shabaab waliingia katika eneo hilo na kuanza kufyatua risasi na kutupa mabomu ya mkono kwa maafisa wa ulinzi katika uwanja wa ndani. Askari wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) walifika katika eneo la tukio chini ya dakika 15, na mapigano makali yalizuka baina yao na wanamgambo kwa zaidi ya saa moja.
Washambuliaji hao, hata hivyo, walishindwa kuingia ndani ya ofosi yoyote na kujilipua wenyewe walipoishiwa na risasi, mashuhuda waliiambia Eroman Informations, na kuongeza kwamba mmoja wa wanamgambo wa al-Shabaab alikamatwa akiwa hai.
Sadiyo Muse, mwenye umri wa miaka 32 na mkaazi katika kitongoji cha Taleh cha Hodan, alisema kuwa dakika chache kabla ya mlipuko kutokea alikuwa amezungumza na baba yake ambaye alikuwa anatembea mbele ya majengo hayo akiwa njiani kwenda kutembelea jamaa wanaoishi karibu.
Muda mchache baada ya mlipuko, jamaa yake alimweleza kuwa majengo ya UN yameshambuliwa na hivyo akakimbilia eneo la tukio.
"Niliutambua mwili wa baba yangu uliokuwa umeungua mbele ya lango kwa nguo zake," aliiambia Eromaninfo.
"Nimeshtushwa sana na kutishwa na kile kilichotokea mjini Mogadishu leo," alisema Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa UN kwa Somalia Nicholas Kay. "Eneo la Pamoja la UN lina wafanyakazi wanaofanya kazi katika masuala ya ubinadamu na maendeleo kwa watu wa Somalia. Hili lilikuwa tendo la kigaidi na jaribio la kukata tamaa la kuigonga Somalia nje ya njia yake ya kurejea kwa hali na ujenzi wa amani."
Mamia ya wafanyakazi wa UN wanafanya kazi katika majengo haya, iliyo na ofosi kadhaa ya mashirika ya UN yakiwemo ya Shirika la Chakula na Kilimo, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, kamishna Mkuu wa UN wa Wakimbizi, na Afosi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu.
Mashirika mengine ya UN, ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Kuokoa Watoto, ambao pia una ofosi zake hapa, za majengo kumi ya gorofa tatu. Wakati wa mapigano ya wazi, waajiriwa walikuwa wamejifungia chini na walikaa mbali na madirisha.
Al-Shabaab ilidai kuhusika na shambulio hilo kupitia Twitter.
"Kitengo cha Mujahidina kutoka Brigedi ya Ushahidi kimevamia eneo la UNDP karibu na uwanja wa ndege mjiini Mogadishu," ilisema siku ya Jumatano.
"Umoja wa Mataifa, mfanyabiashara wa kifo na nguvu ya shertani mwovu, mwenye rekodi nyingi za fedheha za kutoeneza chochote zaidi ya umaskini, utegemezi na ukafiri," al-Shabaab walisema katika jaribio la kuhalalisha umwagaji damu na upotevu wa maisha.
"Mashambulio haya yasiyo na mafanikio ya al-Shabaab yanadhamiria tu kwenye kuvuruga jitihada zinazoendelea za watu wa Somalia kujiondoa katika miaka ya vurugu nchini Somalia na hautazuia kwa kutia hofu jitihada za pamoja kuendelea kusaidia watu wa Somalia kujenga tena nchi yao," alisema Mwakilishi Maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa balozi wa Somalia Mahamat Saleh Annadif.
Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon pia amelaani shambulio hilo muda mchache baadaye.
"Ninalaani shambulio lisilo na maana na baya kwa raia wasio na hatia wa Umoja wa Mataifa asubuhi hii," alisema katika kauli yake. "Umoja wa Mataifa ni rafiki na washirika wetu, na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanatupea msaada wa kibinadamu na usaidizi, hivyo, mimi na Wasomali wote tumeshtushwa kwamba wamekuwa walengwa na waathirika wa vurugu hizo za kikatili."
Ofosi ya waziri mkuu na Umoja wa Mataifa hazikuweza kuthibitisha idadi ya waliouwawa au majeruhi siku ya Jumatano.
"Kwa huzuni tunapaswa kusubiri kusikia maelezo kamili na uthibitisho wa waliouwawa au majeruhi yeyote," alisema Shirdon. "Mawazo yetu yote na sala ni pamoja na wenzetu wa UN leo. Lakini al-Shabaab hawataiangusha mchakato wa amani. Hawatasimamisha ahueni wetu. Vurugu hazitashinda."
Shambulio kubwa la mwisho la al-Shabaab huko Mogadishu lilikuwa mwezi Aprili, wakati kikosi cha makomando wa kujitoa muhanga walipojilipua wakiwa njiani kuelekea kwenye jengo la mahakama kuu ya mogadishu, na kusababisha vifo vya watu 29.
"Wasomali wanawakataa al-Shabaab. Wakati sisi na UNSOM tunaijenga upya Somalia, hawaleti chochote zaidi ya maumivu na uharibifu. Mungu atawalaani," Shirdon alisema katika mtandao wa Twitter.
source AFP

No comments:
Post a Comment