PRESIDENTIAL PREPARATION -3
PRESIDENTIAL PREPARATION - 2
PRESIDENTIAL PREPARATION -1
Ndani ya siku chache zijazo chama chetu kitakamilisha chaguzi zake za ndani, zoezi ambalo limechukua takribani mwaka mzima, tangu chaguzi za kwenye mashina zilipoanza. Zoezi hili litakapo kamilika katika mkutano mkuu wa chama chetu, chombo ambacho ni cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, kitakuwa na uongozi mpya katika nafasi zote.
Baada ya kumaliza kikao chake na wajumbe watarajiwa wa
kamati
kuu ya chama, Robert maarufu kama Robby alirudi ofisini kwakwe, na
kumkuta secretary wake Anna akiendelea kuchapa kazi kama kawaida. Anna
alimsalimu bosi wakena salaam ile ilitikiwa na Robert huku ikifuatiwa na swali,
“there is any problem?”Anna alijibu”hakuna tatizo bosi”okey, hakikisha unampigia
simu Mr. Minja na umwambie ninamuhitaji ofisini kwangu. Maagizo yale aliyo
yaacha Robert yalikubaliwa na Anna, kwa kusema sawa bosi.Robert aliingia
ofisini kwakwe na kuendelea nashughuli zake za kutafuta udhamini kwa watu na
makampuni mbalimbali ndani na hata nje ya nchi, kwa ajili ya kupata pesa ya
kutosha kuwezesha Mheshimiwa Leonard kuingia madarakani.

Kipindi hicho Anna aliendelea kupiga simu ya Mr. Minja bila
kupokelewa.Baada ya kujaribu kupiga simu ya Mr. Minja kwa muda mrefu bila
mafanikio yoyote, Atimaye alimpigia simu bosi wake na kumueleza kwamba simu ya
Mr. Minja ilikuwa inaita bila majibu.“okey, nitamtafutabaadaye ” Robert alimjibu Anna, na kuamua yeye mwenyewe
kumpigia simu Mr. Minja, simu ile iliyopigwa na Robert ilipokelewa moja kwa moja na Minja,
nilimwagiza Anna akupigie simu, lakini simu yako iliita tu bila kupokelewa,
“nikweli mzee nilikuwa na kikao kidogo na wafanyakazi wangu kwa muda wa
kama saa moja hivi” alisema Minja.
Aliendelea Robertkuuliza kama kulikuwepo na tatizo lilopelekea Minja kuitisha
kikao na wafanyakazi wake na Minja
alimjibu moja kwa moja kwamba walikuwa wakipeana utaratibu tu wa kufanyakazi,”
okey, nakuhitaji ofisini kwangu sasa hivi”alisema Robert.
Robert alibaki anawaza kidogo na kukumbuka juu ya utendaji
wa bwana Minja ulivyo mzuri kwa kuibua chokochoko za serikali na chama chetu
kwa ujumla na kuifanya jamii ya nchi yetu kuliamini sana gazeti lake kuliko
chombo kingine chochote cha habari hapa nchini. Ghafla Anna aliingia ofisini kwa Robert na kumfanya Robert ashituke kidogo, “Bosi kuna hili faili la Mr.
Kombani linahitaji lisainiwe, ili baadaye alete cheki” Anna alimwambia bosi
wake, nakuulizwa kama Kombani alifika ofisini, “hakuweza kufika ila alipiga
simu na kusema atakuja baadaye kuchukua hili faili”. Muda huo huo Minja alifika
ofisini kwa bwana Robert, na kusalimiwa na Anna, baadaye na kuondoka na faili
lake baada ya Robert kulisaini. Robert
alimkaribisha Minja na kumwambia “bwana nimekuitia jambo moja tu, na
tena ni la muhimu sana, kipindi hicho Minja alikuwa akimusikiliza kwa umakini
sana alichokuwa akikizungumza Robert, nahitaji umchafue Mheshimiwaaaaaa……mlango
ulifunguliwa na Anna aliingia na kumwambia Robert bosi kuna karatasi moja hujaisaini.

JIONI ya siku hiyo Robert alipita kwa mheshimiwa Leornard, na
kuonana naye na kumueleza hali halisi jinsi kikaoKilivyoenda na maazimio ya
waheshimiwa wajumbe juu ya kikao kile, na kumuleza kwamba wajumbe wote wa kikao
wameazimia juu ya kutafuta ufadhili wa kutosha wa kisi cha zaidi ya bilioni 500
za Kitanzania, ili mambo yote yaweze kwenda vizuri, na kusema kwamba hii nchi
ni kubwa sana kwa mfano kama uchaguzi mmoja wa ubunge tu IGUNGA mkoani Tabora
chama kilitumia Bilioni 6, je, kwa nchi nzima tutatumia pesa kiasi gani? Kutosha
kukata kiu ya watu mbalimbali.Maazimio yale yaliungwa mkono moja kwa moja na
mheshimiwa Leornard, na kusema sasa itabidi tugawane majukumu katika zoezi la
kukusanya fedha, alisema mheshimiwa Leonard. Baada ya mazungumzo ya muda kati ya
mheshimiwa Leornard na Robert. Robert aliamua
kuondoka na kurudi nyumbani kwakwe na kumkuta mke wake na mwanaye mdogo wa
miaka 5, wakiwa salama na kuingia bafuni kuoga.
PRESIDENTIAL PREPARATION - 2
Piiiiiiiiiiiiiiiii,piiiiiiiiiiiiiiiiii,piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,
ilikuwa ni honi ya gari inapigwa getini kwa mheshimiwa Leornard, na
kumfanya
mlinzi aende kuchungulia nani alikuwa
anapiga honi getini. Lakini wakati baba
askofu anafika getini kwa mheshimiwa Leornard tayari Alisha mtaarifu kama
kafika, wakati mlinzi anachungulia getini, simu yake ya kibandani iliita na alipoipokea, aliambiwa
na mheshimiwa Leornard amfungulie baba askofu. Mlinzi alirudi getini na
kumfungulia Baba Askofu. Baada ya kuingia ndani Baba askofu aliegesha gari yake
, sehemu ya maegesho ya magari nyumbani kwa mheshimiwa
Leornard na alipo shuka
kutoka kwenye gari alimsalimia askari Yule wa getini. Na baada ya salamu askari
Yule alimuongoza Baba Askofu mpaka alipokuwa amekaa mheshimiwa Leornard na Mzee Anthony.
Mheshimiwa Leornard: Oooooh Baba Askofu karibu sana.
Baba Askofu: Asante sana, tumsifu yesu kristo. Mheshimiwa
Leornard kwa pamoja na Mzee Anthony: waliitikia milele amina.
Baada ya kujuliana hali za majumbani mwao wote watatu kwa
pamoja, Silyvia mfanyakazi wa nyumbani kwa mheshimiwa Leornard alifika na
kumsalimu baba askofu, na kumuuliza kinywaji ambacho angependa kutumia, kipindi
hicho mheshimiwa na mzee wa kanisa mzee Anthony walikuwa wakiendelea kunywa
juice na baba askofu aliomba aletewe maji ya kunywa ili aweze kupooza koo.
Baada ya muda mfupi mama Lawrence, mke wa mheshimiwa Leornard alitoka ndani
akiwa na maji na kwenda kumuhudumia baba askofu, na kusalimiana kidogo na mama
Lawrence alirudi ndani na kumuacha mheshimiwa Leonard, Baba Askofu pamoja na
mzee Anthony wakiendelea na mazungumzo yao.
Mzee Anthony; aaaaah Baba Askofu, baada ya misa ya juzi
kuona umezungumzia sana swala la michango na sadaka kwa ujumla kwa wauminii……….Baba
Askofu: ndiyo ndiyo

Mzee Anthony: nilifikilia sana na kujiuliza maswali mengi ni
kivipi kupitia tu sadaka tungeweza kumalizia ujenzi ambao umebakia, tena ambao
ni mkubwa kuliko sehemu tuliyojenga, “ni kweli mzee wa kanisa” yalikuwa ni
maneno yake baba askofu. Niliamua kumfuata Mheshimiwa Leornard hapa,
nikamuelezea hali halisi juu ya sehemu ya ujenzi wa kanisa letu ulipofikia, na
yeye kwa upande wake amehaidi kuchangia milioni 100 pesa za kitanzania.
Abarikiwe na Mwenyezi Mungu atamlipa alisema baba askofu. Aliendelea mzee wa
kanisa kwa kusema, lakini wakati tukiyazungumza haya, shemeji mama Lawrence
naye alikuwepo na akashauri kwamba mheshimiwa Leonard ni mtu wa watu
anayependwa sana na watu, kwahiyo ingekuwa vyema ahudhurie ibada na kufanya
harambee kwa waumini ili tukamilishe
ujenzi wa nyumba ya ibada, naimani waumini wataweza kumsikiliza kiongozi wao
kwasababu wanampenda na wanaweza kumalizia kiasi kilichobaki.
Baba Askofu : Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, wazo
zuri sana mzee wa kanisa, naimani haya yote ni mapenzi mema ya mwenyezi Mungu
juu ya nyumba yake ya ibada. “nikweli baba askofu ”alisema mheshimiwa Leornard.
Karibu sanamheshimiwa Leonard kanisani kwetu kwa ajili ya huduma za kiroho na
kuwahamasisha waumini juu ya ujenzi wa nyumba yao ya ibada.
PRESIDENTIAL PREPARATION -1
Ndani ya siku chache zijazo chama chetu kitakamilisha chaguzi zake za ndani, zoezi ambalo limechukua takribani mwaka mzima, tangu chaguzi za kwenye mashina zilipoanza. Zoezi hili litakapo kamilika katika mkutano mkuu wa chama chetu, chombo ambacho ni cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, kitakuwa na uongozi mpya katika nafasi zote.
Kutakuwepo na viongozi wapya kabisa, watakuwepo na waliorudi
na wapo ambao watakuwa wamebadilishwa nafasi zao. Wapo wale ambao licha ya
kujaribu sana watakuwa wametupwa kwenye nafasi za uongozi ndani ya chama hata
kama wanazo nafasi zao za kiserikali.
Viongozi hawa wapya watakao chaguliwandio watakao kuwa wajumbe
wa mkutano mkuu wa chama chetu, mkutano mkuu wa chama ndicho chombo cha juu
kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, upo juu ya vyombo vingine vyote ,
ikiwemo katiba ya chama chetu, kwani ndicho chombo ambacho kinaweza kubadili
katiba ya chama bila kuwa na rufaa dhidi yake. Lakini zaidi ni mkutano mkuu
ndio ambao unaweza kutengua uamuzi wowote uliowahi kutolewa kipindi cha nyuma
na chombo chochote au na mtu yeyote wa chama chetu. Kimsingi mkutano mkuu
unaweza kutengua maamuzi ya sekretarieti ya chama au hata ya mwenyekiti wa
chama chetu.
Kwahiyo kuelekea uchaguzi huu mkuu lazima kambi yetu
ijipange kuhakikisha sekritarieti yote ya chama inatuunga mkono na theluthi
mbili ya wajumbe wote wa mkutano mkuu wanakuwa ni wakambi yetu ndani ya chama.
Kwasababu kuelekea uchaguzi mkuu mara baada ya uchaguzi
ndani ya chama chetu ni lazima
tutashuhudia kuibuka angalau kwa kambi mbili zaidi, ukiondoa kambi yetu ya
mheshimiwa Leornard. Kambi hizi mbili za
ziadazitasabisha msuguano ndani ya chama chetu, kama tulivyo shuhudia katika
uchaguzi mkuu wa nchi uliopita. Japokuwa uwezekano mkubwa wa kambi moja kati ya
hizi mbili kujitoa ndani ya chama chetu . Hili litategemea jambo moja kubwa,
kupatana kwa mheshimiwa Leonard na kambi ya mheshimiwa Seba, endapo tutashuhudia
viongozi wetu hawa wakiamua kupatana na hatimaye kusimama pamoja, basi mgombea
wa chama chetu ambaye atakuwa ni mheshimiwa Leonard atashinda kwa kishindo
katika uchaguzi mkuu wa nchi ujao.
Lakini ukweli ni
kwamba majeraha ya kashifa ya ufisadi hayawezi kuponyeka kwa
kukumbatiana au kwa kupiga picha pamoja, majeraha haya kwa mheshimiwa Leonard
yamezama sana kiasi kwamba sioni uwezekano wowote wa kambi za chama chetu
kuweza kukaa pamoja, ni lazima mwenye nguvu apishwe na atakapopita wanaobakia
ni lazima watoke.
Written by: Lincoln Pascal 2012.
Don't miss every Thursday and Monday.
#################################################################################
No comments:
Post a Comment