PRESIDENTIAL PREPARATION -1
#################################################################################
Ndani
ya siku chache zijazo chama chetu kitakamilisha chaguzi zake za ndani, zoezi
ambalo limechukua takribani mwaka mzima, tangu chaguzi za kwenye mashina zilipoanza.
Zoezi hili litakapo kamilika katika mkutano mkuu wa chama chetu, chombo ambacho
ni cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, kitakuwa na uongozi mpya
katika nafasi zote.

Kutakuwepo na viongozi wapya kabisa, watakuwepo na waliorudi
na wapo ambao watakuwa wamebadilishwa nafasi zao. Wapo wale ambao licha ya
kujaribu sana watakuwa wametupwa kwenye nafasi za uongozi ndani ya chama hata
kama wanazo nafasi zao za kiserikali.
Viongozi hawa wapya watakao chaguliwandio watakao kuwa wajumbe
wa mkutano mkuu wa chama chetu,
mkutano mkuu wa chama ndicho chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama chetu, upo juu ya vyombo vingine vyote , ikiwemo katiba ya chama chetu, kwani ndicho chombo ambacho kinaweza kubadili katiba ya chama bila kuwa na rufaa dhidi yake. Lakini zaidi ni mkutano mkuu ndio ambao unaweza kutengua uamuzi wowote uliowahi kutolewa kipindi cha nyuma na chombo chochote au na mtu yeyote wa chama chetu. Kimsingi mkutano mkuu unaweza kutengua maamuzi ya sekretarieti ya chama au hata ya mwenyekiti wa chama chetu.

Kwahiyo kuelekea uchaguzi huu mkuu lazima kambi yetu
ijipange kuhakikisha sekritarieti yote ya chama inatuunga mkono na theluthi
mbili ya wajumbe wote wa mkutano mkuu wanakuwa ni wakambi yetu ndani ya chama.

Kwasababu kuelekea uchaguzi mkuu mara baada ya uchaguzi
ndani ya chama chetu ni lazima
tutashuhudia kuibuka angalau kwa kambi mbili zaidi, ukiondoa kambi yetu ya
mheshimiwa Leornard. Kambi hizi mbili za
ziadazitasabisha msuguano ndani ya chama chetu, kama tulivyo shuhudia katika
uchaguzi mkuu wa nchi uliopita. Japokuwa uwezekano mkubwa wa kambi moja kati ya
hizi mbili kujitoa ndani ya chama chetu . Hili litategemea jambo moja kubwa,
kupatana kwa mheshimiwa Leonard na kambi ya mheshimiwa Seba, endapo tutashuhudia
viongozi wetu hawa wakiamua kupatana na hatimaye kusimama pamoja, basi mgombea
wa chama chetu ambaye atakuwa ni mheshimiwa Leonard atashinda kwa kishindo
katika uchaguzi mkuu wa nchi ujao.
Lakini ukweli ni
kwamba majeraha ya kashifa ya ufisadi hayawezi kuponyeka kwa
kukumbatiana au kwa kupiga picha pamoja, majeraha haya kwa mheshimiwa Leonard
yamezama sana kiasi kwamba sioni uwezekano wowote wa kambi za chama chetu
kuweza kukaa pamoja, ni lazima mwenye nguvu apishwe na atakapopita wanaobakia
ni lazima watoke.
Written by: Lincoln Pascal 2012.
Don't miss every Thursday and Monday.
#####################################################################################
No comments:
Post a Comment